Msanii nyota wa Bongo fleva, Naseeb Abdul Juma maarufu kama Diamond Platnumz amezindua rasmi bidhaa yake ya manukato inayoitwa ‘Chibu Perfume’.

Diamond amezindua manukato hayo leo Aprili 21, 2017 jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa perfume hiyo imetengenezewa Dubai na pia ametangaza jinsi ya kuipata pamoja na gharama yake itakayouzwa.

Aidha, Diamond amewataka wasanii wengine kuamka na kutumia umaarufu kujiimalisha katika maendeleo na kufanya vitu vyenye tija katika jamii kama yeye anavyofanya badala ya kusubiri wanasiasa wafanye.

Video: Quick Rocka aachia ‘Down’ aliyompa shavu la kwanza Mimi Mars
Video: Majaliwa asema Dkt. Elly alitoa mchango mkubwa