Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini, Diamond Platinumz ambaye anafanya vizuri katika sanaa ya muziki, anaendelea kuonesha umahiri katika kazi yake kwa kuendelea kukuza na kutanua soko la ajira Tanzania kwa ujasilia mali.

Hivi karibuni ametambulisha ujio wa kituo chake cha radio, Wasafi Fm, na kituo cha TV cha Wasafi TV.

Harakati hizo zipo mbioni kukamilika mara baada ya kutumia ukurasa wake wa instagram kuonesha mitambo mbalimbali ambayo tayari imefungwa kuruhusu chaneli hizo kuanza rasmi kurusha vipindi vyake.

Diamond Platinumz ambaye hivi karibuni amekabiliwa na majanga makubwa ya kuachwa kimapenzi na  mama watoto wake Zarina Hassan.

Hivyo katika kipindi hiki cha maombolezo ameamua kujikita zaidi katika kazi, hilo amelithibitisha kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo ametangaza tarehe, 16 machi mwaka huu kuzindua rasmi albamu yake ya A boy From Tandale.

Ambapo uzinduzi huo umetangazwa pia kufanyika katika baadhi ya miji Marekani kuanzia juni 22 hadi julai 23, ambapo ametaja miji hiyo kuwa ni , New York, Atlanta, Columbus, Dallas, Boston, Seattle, Minnesota, Kansas City, Huoston, Los Angeles na Washngtn DC.

Amesema kuelekea uzinduzi huo wa albamu amewaomba waliopo Marekani katika miji hiyo wajiandae kwa ziara hiyo ya A Boy From Tandale.

 

 

Israel yaonya kuipiga Iran, yatungua ndege yake isiyo na rubani
Wolper: Tanzania jina la nchi yetu naona si tamu tena na limeanza kuwa chungu