Mkuu wa Wilaya ya Arumeru iliyopo mkoni Arusha, Jerry Murro amwatahadharisha baadhi ya madiwani ambao wametanguliza maslahi yao binafsi kuliko kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.

DC Murro amewataka madiwani hao kuondoa tofauti zao za kiitikadi za vyama na waungane kuwatumikia wananchi na si kwa kutanguliza maslahi binafsi au vyama vyao wanavyovitumikia.

Amesema kuwa malumbano siku zote huwa hayajengi bali huchelewesha na kurudisha nyuma maendeleo na kusababisha migogoro kwa wananchi wanaowatumikia katika maeneo yao.

“Natoa tahadhari kubwa kama mtaendelea na malumbano yasiyokuwa na tija kwa wananchi, nitamuomba waziri mkuu aje avunje baraza hili la madiwani, maana kuna baadhi yenu humu wametanguliza matumbo mbele kuliko kutatua miogogoro ya ardhi inayowakabiri wananchi,”amesema Murro

Breaking News: Julius Mtatiro ajivua uachama CUF, ajiunga na CCM- Video
Video: Fredy Lowassa aleta mafuriko Monduli, Unyama wa Polisi kwa Mwandishi wazua taharuki

Comments

comments