Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa ameagiza kukamatwa mara moja kwa mtu mmoja aliyekuwa akiwahifadhi mabinti kwa lengo la kuwasafirisha kwenda Uarabuni kwa ajili ya kufanya kazi za ndani.

Ametoa agizo hilo hii leo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Kibada lililopo wilayani Kigamboni.

Amesema kuwa tabia kama hiyo haikubariki hata kidogo kwani mabinti wengi ambao wamekuwa wakirubuniwa kwenda kufanyakazi Uarabuni wamekuwa wakiishia kupata matatizo.

“Nasema tabia kama hii lazima tuikomeshe, naagiza mtu huyu akamatwe mara moja, huu si utu hata kidogo, kila siku mabinti zetu wanataabika huko Uarabuni,”amesema Mgandilwa

Video: Dkt. Ndugulile azindua kampeni ya zimamoto mlango kwa mlango
Makonda aagiza mwanafunzi aliyepotea ashughulikiwe