Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela amesema kuwa anajivunia kubadili fikra za wananchi wa wilaya hiyo kuwa wajasiliamali.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kitu kikubwa alichokifanya mara baada ya kuwasili alibadili fikra za wananchi hao.

Amesema kuwa baada tu ya kufika kazi ya kwanza ilikuwa ni kuanza kufundisha ujasiliamali hivyo kubadili fikra za wananchi katika suala zima la biashara.

Aidha, ameongeza kuwa vitu alivyovifanya ni vikubwa na vya kujivunia kwakua kubadili fikra za mtu na kuleta maendeleo sehemu husika si kazi ndogo.

“Hivi vyote nikivikumbukaga huwa vinanifanya nijisikie raha kwasababu, hakuna kitu kizuri katika maisha kama kufanya kitu cha kukumbukwa,”amesema Kasesela

 

 

Afya ya Mbowe yaimarika,..'hapumulii mashine tena'
Township Rollers: Tunaifahamu vizuri Yanga