Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba Classic ameachia ngoma mpya akiwa amemshirikisha Vanessa Mdee inayoenda kwa jina la Chausiku.

Wimbo huo unaonekana kufanya vizuri tangu kuachiwa kwake rasmi, na sasa umeshika nafasi ya 5 katika mtandao wa You Tube katika nyimbo zinazofanya vizuri na zilizoongoza kutazwa kwenye mtandao huo.

Aidha wawili hawa mbali na kazi hii ya Chausiku, wamewahi kufanya kazi nyingine iliyoenda kwa jina la ‘Siri’ ambayo ilifanya vizuri katika kiwanda cha muziki nchini mwaka 2015, na katika nyimbo hizi mbili namna ya uimbaji wao umekuwa ni mmoja wa kujibizana unaowavutia wasikilizaji wengi kusikiliza kazi yao.

Kuutazama wimbo huo ambao safari hii wamekuja kiuswazi zaidi akiwemo Dulla Van mchekeshaji aliyepata umaarufu kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa upekee wa maigizo yake.

Bonyeza kitufe chekundu hapa chini kutazama.

Mpina aomba radhi maofisa wake kupima samaki kwa rula
Kinda la U21 Ufaransa latua West Ham Utd