Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataka viongozi vijana waliopo serikalini kufuata maadili ya kazi zao na si vinginevyo.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati wa upigaji wa kura ya kupitisha bajeti kuu, ambapo amesema kuwa kuna kiongozi mmoja ambaye amekuwa akitumia cheo chake vibaya.

Ndugai ameshauri kuwa ni bora viongozi hao wakafuata maadili ya kazi kuliko kutanguliza mihemko na kujipendekeza kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumpelekea maneno ambayo hayana msingi wowote.

”Kama kuna mtu ana deni kubwa la kufanya kwa hawa wachezaji ni yeye, sitaki kusema lakini leo ngoja niishie hapa, huyu kiongozi amekuwa muongo sana, anamdanganya Rais wa nchi hadharani, mbele ya wananchi, viongozi wa aina hii inabidi wafundwe,”amesema Spika Ndugai

 

Video: JPM aikingia kifua Taifa Stars, 'Kwenye mpira lolote linaweza kutokea'
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 26, 2019

Comments

comments