‘Video Vixen’ aliyegeuka kuwa moja kati ya wakali wa Bongo Fleva, Amber Lulu amezungumzia safari ya uhusiano wake na Harmorapa ilipoanzia na ushauri wake kwa rapa huyo.

Akizungumza ‘exclusively’ na Dar24 hivi karibuni, Amber Lulu ameyakumbuka mazingira waliyokutana na rapa huyo na maongezi yao ya awali huku akifafanua jinsi ambavyo rapa huyo alivyomsifia.

Alisema wawili hao walikutana kwenye studio za mtayarishaji wa muziki, Mr. T-Touch na rapa huyo alifunguka jinsi anavyomkubali na kisha kupeana mawasiliano.

Angalia video hii kupata undani wa uhusiano walionao na ushauri wake kwa rapa huyo:

 

Katika hatua nyingine, Amber Lulu amesema kuwa anatarajia kuachia wimbo wake mpya hivi karibuni alioubatiza jina la Only You.

“Wategemee video yangu mpya ambayo iko tayari audio na video. Wategemee kuiona hewani hivi punde,” Amber Lulu aliiambia Dar24.

Wakazi wa Kata ya Mabilioni hatarini kupata maambukizi
Trump: Jeshi la Marekani liko tayari kuishambulia Korea Kaskazini

Comments

comments