Baada ya siku 10 tangu kukamatwa kwa rapper 21 Savege na idara ya uhamiaji nchini Marekani amekaa kuzungumzia sakata lake kwa mara ya kwanza ambalo limeendelea kuviteka vichwa vya habari  duniani.

Kwenye mahojiano na Goord Morning America kwenye kipande kilichowekwa mtandaoni Amesema kwamba ulikuwa ni mtego au mpango wa maafisa hao wa uhamiaji kumtia nguvuni kwani hata wakati anakamatwa hawakumwambia chochote zaidi walisikika wakisema Tumempata 21 Savage.

Hata hivyo sakata hilo linahusishwa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa mujibu wa tovuti ya TMZ imeripoti kuwa Trump yupo nyuma ya ishu hii na anachochea Savege arudishwe Uingereza.

Rapper huyo anaetamba na kibao cha ‘A lot’ alikamatwa na polisi akiwa anaendesha gari kwa mwendo kasi huku akiwa amebeba silaha kwenye gari lake ambayo ilikuwa imejaa risasi za kutosha ni kwa mujibu wa taarifa za polisi.

Aidha savage anakabiliwa na mashtaka ya dawa za kulevya  pamoja na kuishi nchi Marekani kinyume na sheria, makosa ambayo yangejumuishwa yangeongezea zaidi rapper huyo kutimuliwa Uingereza ambapo siku ya jana kaachiwa kwa dhamana.

Moja kati ya mastaa wakubwa nchini Marekani Jay Z alijitokeza na kuajiri mwanasheria Alex Spiro  kusaidia kwenye kesi ya 21 Savage, kama ilivyokuwa kwa Meek Mill alopokuwa amefungwa Hov alimsaidia kwa kiasi kikubwa kwenye kesi yake “mbali na kuwa msanii mkubwa ana haki ya kulea watoto wake”Alisema Jay Z.

 

 

Video: Tamaduni za kushangaza zaidi siku ya Valentine
Zaidi ya watoto 100,000 hufariki kwenye vita kila mwaka

Comments

comments