Mwanadada anayefanya vizuri katika sanaa ya muziki wa Bongo Fleva na sasa anafanya vizuri katika mauzo ya albamu yake inayojulikana kama MoneyMonday, Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money ametaja gharama alizotumia kukamilisha albamu hiyo.

Ambapo amesema kuwa albamu ya MoneyMonday mpaka kukamilika imemgharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania Milioni 100.

”Nimetumia fedha nyingi lakini kwangu sioni tatizo lolote, niliangalia zaidi jinsi gani watu watatambua Vanessa kafika wapi katika kukua kimuziki, fedha hiyo nililipa idara zote kuanzia wasanii walioshiriki matangazo, video nk na bado naendelea kutoa kwa kuwa matangazo bado yanaendelea ,” amesema Vanessa.

Ameongezea kuwa hajutii matumizi ya kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kuwa lengo lake hasa ni kutoa kazi itakayomwongezea heshima kwenye muziki wake sambamba na kuhakikisha inawifikia watu wa aina zote.

Hivi karibuni Vanesa ameachia albamu yake katika ukumbi wa Mlimani City.

Vanessa ni kati ya wasanii wachache ambao wanajaribu kurudisha utamaduni wa kutengeneza Albamu katika muziki wa Bongo fleva jambo ambalo kwa siku za nyuma limekuwa likififia na kupotea.

Msanii mwingine mwenye ujasili wa kurudisha utamaduni wa wasanii kutengeneza albamu ni Diamond Platinum ambaye naye hivi karibuni ataachia albamu yake ya mtoto wa Tandale ambapo juzi alitaja baadhi ya sababu zilizomfanya acheleweshe kutoka kwa albamu hiyo.

 

Masau Bwire awaomba radhi wanasimba
Mpango wa Trump kuboresha nyuklia walaaniwa vikali