Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Sven Vandenbroeck, amesema anaamini ligi kuu ya Tanzania Bara itaweza kumalizika baada ya changamoto ya Corona kupita.

Vandenbroeck amesema kwa sasa ni mapema sana kufikiria uamuzi huo “Nina imani kutakuwa na muda wa ligi kuweza kumalizika, kwa sasa ni vyema kulinda maisha ya kila  mmoja wetu kutokana na janga hili la Corona,” amesema Sven “Kufikiria kufuta ligi sasa ni mapema sana, tuziache mamlaka zifanyie kazi changamoto iliyopo kwanza”.

Sven ametoa maoni hayo siku moja baada ya baadhi ya timu za Ligi Kuu kupendekeza ligi hiyo imalizike sasa.

Kulingana na gazeti la Mwanaspoti, Makamu Mwenyekiti wa Young Africans Fredrick Mwakalebela alipendekeza ligi imalizwe, klabu ya Simba inayoongoza ligi ikabidhiwe ubingwa huku akipendekeza klabu ya Azam Fc ambayo inashikilia ubingwa wa kombe la shirikisho (ASFC) ipewe nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika pamoja na Simba.

Tanzania waongezeka wagonjwa wapya wanne wa Corona
Rais Kenyatta apiga marufuku usafiri Nairobi kupambana na corona