Klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki, imeweka wazi matamanio ya kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Man Utd, Robin van Persie.

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uturuki, Yalcin Kaya amethibitisha suala hilo kwa kusema tayari wameshamzungumza mshambuliaji huyo katika vikao vyao kwa zaidi ya mara mbili na kinachoendea sasa ni mipango ya kuwasilisha ofa ya usajili wake huko Old Trafford.

Kaya, amesema wanaamini Van Persie atawafaa baada ya kuondoka kwa mshambuliaji kutoka nchini Senegal, Demba Ba ambaye mwanzoni mwa juma hili alikamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Besiktas huenda ukapata changamoto ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, kutokana na kuendelea kujiamini bado anastahili kwenye kikosi cha mashetani wekundu chini ya utawala wa meneja kutoka nchini Uholanzi, Louis Van Gaal.

Endapo mipango ya klabu ya Besiktas itakamilishwa kama ilivyopangwa na bodi ya wakurugenzi, huenda ikawa sehemu ya klabu za nchini Uturuki ambazo zikazowasajili mchezaji kutoka Man Utd.

Viongozi wa klabu ya Fenerbahce kupitia kwa mkurugenzi wao wa michezo Guilliano Terraneo wapo katika mazungumzo ya kumsajili Luis Nani ambaye alipekwa kwa mkopo Sporting Lisbon msimu uliopita.

Uvumilivu Wamshinda Mancini, Amruhusu Shaqiri Kuondoka
Lowasa: Anaesema Mimi Mla Rushwa Alete Ushahidi