Mshambuliaji Mathieu Valbuena amekubali kurejea nyumbani Ufaransa na kujiunga na klabu ya Olympic Lyon kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, amejiunga na Lyon iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye msiammo wa ligi ya Ufaransa msimu uliopita, akitokea nchini Urusi alipokua akiitumikia klabu ya Dynamo Moscow.

Valbuena alijiunga na Dynamo Moscow miezi 12, iliyopita kwa ada ya usajili wa paund million 6 akitokea kwenye klabu ya Olympic Marseille, lakini hali ilikua tofauti nchini Urusi na kufikia hatua ya kukubali kurejea nchini kwao Ufaransa.

Valbuena, amesema katu hatojutia nafasi ya kucheza soka nchini Urusi aliyoipata kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita, na anaamini maamuzi aliyo yachukua ya kurejea nyumbani ni sahihi kwake pamoja na kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa klabu yake mpya.

Amesema anatambua malengo la Olympic Lyon katika msimu wa 2015-16 na ndio maana amekubalia kujiunga nao, kutokana na hitaji la kutaka kurejesha heshima ya kutwaa ubingwa wa nchini Ufaransa ambao kwa sasa unashikiliwa na PSG kwa misimu mitatu mfululizo.

Usajili wa Valbuena utaisaidia Olympic Lyon kuziba nafasi ya Alexandre Lacazette ambaye aliumia mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ufunguzi wa ligi ya Ufaransa.

Makubaliano Ya Ndoa Ya TFF Na Vodacom
Wenje Azungumzia Ujio Mpya Wa Dk. Slaa