Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amejibu tuhuma za mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na kumtaka asipotoshe wananchi bali apeleke malalamiko yake kwenye kamati.

Ameyasema hayo hii leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akiendesha kikao cha bunge, na kusema kuwa bunge lina utaratibu wake kwenye kila jambo linalohusika bungeni hapo hivyo malalamiko yote yanatakiwa yapelekwe kwenye kamati.

“Lema asipotoshe wananchi aende hadharani kwenye kamati kuzungumzia hayo, bunge haliwezi kusimama kwa shambulio la Lissu bali kanuni zinasema mbunge akifariki bunge linasimama kwa siku moja. na iwapo Spika akiletewa jambo la maadili linapelekwa kamati ya maadili, suala la jinai linapelekwa polisi,” amesema Spika Ndugai

Aidha, Ndugai amesema suala la Tundu Lissu kuchangiwa fedha za matibabu na wabunge wakati yeye alitibiwa nje ya nchi ni kwamba matibabu ya Tundu Lissu yameenda kinyume na utaratibu wa bunge.

Hata hivyo, jana mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alimlaumu Spika Ndugai kuwa anashindwa kutetea kiti chake, kwa kuzidi kuwakandamiza wabunge wa upinzani hususani suala la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu.

Taifa Stars yashuka viwango vya FIFA
LIVE: Uzinduzi wa mradi wa kulijengea uwezo Bunge