Staa wa kike wa Bongo Movie, Irine Uwoya siku ya tarehe 18 Disemba alisherekea siku yake yakuzaliwa ambayo alikuwa akiiandika katika ukurasa wake wa instagram ambapo alisema imefanyika  tofauti kidogo.

Msanii huyo ambaye amekuwa anafanya vizuri katika filamu za bongo amabzo ameshirirki na kuipaisha sanaa ya bongo ndani na nje ya Afrika Mashariki.

Aidha, Irine Uwoya katika siku yake hiyo muhimu aliamua kuishereka na makundi maalumu wakiwemo watoto yatima, kina mama na wazee katika viwanja vya leaders club huku ikihudhuriwa na wasanii wenzake mbalimbali pamoja na viongozi wa Serikali.

Sherehe hiyo ya kutimiza miaka 30 kwa Irine Uwoya iliambatana na ufunguzi wa Club yake mpya ambayo inatarajia kufunguliwa mwezi huu Disemba.

Offset aomba msamaha hadharani
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 19, 2018

Comments

comments