Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni, Lilian Rwebangira amesema wamekamata gari la meya wa jiji wa Dar es Salaam kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni likiwa na vijana wawili waliovaa sare za chama.

Ambapo Kamanda wa polisi Kinondoni, Jumanne Murilo amethibitisha kukamatwa kwa gari hilo na kudai uchunguzi zaidi unaendelea.

Tukio hilo limeelezwa kutokea jana mida ya saa mbili na nusu usiku, ambapo dereva wa Meya alohojiwa sababu zakuonekana eneo hilo mida hiyo, na kutaja sababu tofautitofauti kwamba alikwenda kuegesha na sababu nyingine kuwa alimpeleka meya Mwita kwenye mkutano maeneo ya jirani.

Rwebangira amedai kwamba kuonekana kwa gari hilo ni njama za Chadema kutaka kuvuruga uchaguzi wa Februari 17 na kwamba tayari wamefikisha suala hilo katika Kituo cha Polisi Magomeni ambako dereva wake anashikiliwa pamoja na gari hilo.

“Tulipekua simu ya dereva na kubaini mawasiliano kati yake na meya wa jiji akimuuliza “Uko na nani hapo?”, “Mpango unakwendaje?”. Zote hizo ni njama za wenzetu kutaka kuvuruga uchaguzi, sasa tunaliomba jeshi la polisi lifanye kazi yake kwa haki,” amesema Rwebangira.

Hata hivyo, uongozi wa Chadema umekanusha kula njama dhidi ya CCM na kusema kwamba hiyo ni mbinu za chama hicho tawala kutaka kuvuruga uchaguzi.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita hakupatikana mara moja kuzungumzia tukio hilo lakini Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrick Ole Sosopi amesema kwamba jana usiku baada ya kikao cha tathmini Mwita alilalamika kwamba dereva wake haonekani.

 

Tafiti: Waendesha bodaboda wanachangia 13% mimba za utotoni
Bruno Mars afunika Grammy 2018, wanawake walia na usawa