Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amesema kuwa Mgombea Ubunge, Jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu kuwa ni sawa na bibi harusi na kuwa wao CCM watashinda uchaguzi huo.

Amesema kuwa Watanzania wanakipenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati huu kuliko wakati mwingine wowote hivyo ni lazima Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya (CCM), Maulid Mtulia ashinde.

“Kinondoni tunakwenda kushinda nimesikia Kamati ya harusi imemchagua Bibi harusi mmoja, hawa wanacheza siasa ya diblo dibala mara wamo mara hawamo lakini faida tuliyopata safari hii wametuletea mtu mwenye historia ya kushindwa, kaomba Ubunge kwao huko visiwani kapigwa, kaomba Ubunge wa Afrika Mashariki kapigwa na Kinondoni atapigwa, nachohitaji Kinondoni nataka kipigo kitakatifu ili baada ya kushindwa Salum Mwalimu aache siasa atafute biashara nyingine,”amesema James

Hata hivyo, amedai kuwa Salum Mwalimu ni mbuzi wa kafara wa CHADEMA kuwa kila shughuli ngumu wanamtuma yeye ili akafe wao wabaki.

Wananchi kushuhudia chimbuko la binadamu
Wajasiliamali watakiwa kuchangamkia fursa