Hatimaye taasisi ya TWAWEZA imetoa utafiti wake juu ya hali ya siasa nchini zikiwa zimebaki siku 32 kabla ya kupiga kura ya kumchagua rais, wabunge na madiwani.
Kwa mujibu wa tafiti hizo, endapo kura zingepigwa leo, mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli angeshinda kwa asilimia 65 dhidi ya mpinzani wake mkuu kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa, akipata asilimia 25.
Katika utafiti huo, watu 1848 ndio waliohojiwa.
Twaweza: Wananchi wengi wamesema Uchaguzi wa Mwaka 2015 wangempigia kura kwa 65% ya waliohojiwa #SautiZaWananchi pic.twitter.com/RhjBLwNxqX
— Jamii Forums (@JamiiForums) September 22, 2015
Twaweza wameeleza kuwa utafiti huo ulifanywa katika maeneo ya mijini na vijijini na kwamba hawakutaja jina la mgombea bali majina yote yalitajwa na wananchi hao. Hata hivyo, utafiti huo umeonesha kuwa wananchi wengi hawafahamu vyama vilivyosimamisha wagombea urais. Kupitia swali lilikuwa kwenye dodoso likimtaka mwananchi kueleza chama ambacho angekichagua katika nafasi ya urais, vyama vya NCCR Mageuzi, NLD, CUF, na Chadema vinaonekana kwenye jedwali la majibu. Hata hivyo vyama hivyo vilipewa alama ya chini zaidi kulinganishwa na CCM iliyobeba asilimia 60.
Twaweza: Uchaguzi ungefanyika leo, ungempigia kura mgombea wa chama gani? #SautiZaWananchi #Uchaguzi2015 #TZ2015 pic.twitter.com/KXbYYS4EKU
— Jamii Forums (@JamiiForums) September 22, 2015
Kadhalika, matokeo yanayotokana na swali lilikuwa kwenye Dodoso likiwataka wananchi kutaja jina la mgombea urais ambaye ana sifa hizo, ambapo alama za jumla zilionesha mgombea urais kupitia CCM anaongoza.
Twaweza: Wananchi wanadai watamchagua Magufuli sababu ni mchapakazi na Lowassa ataleta mabadiliko #SautiZaWananchi pic.twitter.com/YIdv2sjBCz
— Jamii Forums (@JamiiForums) September 22, 2015
“Ifahamike kuwa, watu wanaweza kubadilisha maamuzi wakati wowote kuanzia sasa kwa jinsi ambavyo Utafiti unaonyesha,” walisema Twaweza.