Wakati mchakamchaka wa kampeni za uchaguzi mkuu unaendelea kushika kasi huku mikutano ya wagombea urais wa CCM na Chadema ikionesha kuvuta umati mkubwa wa tu, utafiti utakaotoa picha ya mshindi unatarajiwa kuwekwa hadharani ndani ya siku 11.

Taasisi zinazoshughulika na tafiti za Twaweza na IPSOS tayari zimesema kuwa tayari zimekamilisha kazi ya kukusanya taarifa na kwamba wanamalizia kuzitafrisi na kuzidadavua ili wawahi ukomo wa siku zilizowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA). Mamlaka hiyo imeweka ukomo wa siku 30 kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu (Oktoba 25).

“Tuko katika hatua za mwisho za kuandaa taarifa na tunatarajia kutoa matokeo ya tafiti ndani ya wiki mbili,” alisema Meneja Mawasiliano Mwandamizi wa Twaweza, Risha Chande.

Kwa upande wa IPSOS-Synovate, walieleza kuwa wanatarajia kutoa matokeo yao ndani ya siku chache zijazo.

Wakati taasisi hizo zikitarajia kutoa matokeo yao hivi karibuni, Mwenyekiti wa taasisi ya REDET, Dr Benson Banna alisema kuwa taasisi yake haikuweza kufanya utafiti mwaka huu kwa sababu za ukosefu wa fedha.

Ahadi Nyingine Ya Lowassa Na Maneno Yaliyowekwa Kwenye Biblia
Bondia Khan Kusaidia Wakimbizi