Mwanamuziki maarufu nchini Marekani Usher Raymond bado anapambana na staka lingine la kumuambukiza ugonjwa wa zinaa mwanadada Laura Helm.

Ni baada ya kumalizana  na kesi ya mwanadada Quantasia Thompsone miezi michache iliyopita

Kwa mujibu wa mtandao wa Bossip umeripoti kuwa Usher anataka taarifa zote juu ya kesi hiyo ziwe siri ya mahakama na wao wawili tuu.

Hivyo ameiomba mahakama ombi maalumu  la kuzuia taarifa za vipimo  vyao na kila kitu ziisitoke  kwenye vyombo vya habari

Aidha, mwanamuziki huyo hataki kuvifaidisha vyombo vya habari, lengo lake ni kulinda ‘brand’ yake  dhidi ya uharibifu wowote na pia kuepuka kudhalilika baina yake na Laura.

Usher bado anakanusha tuhuma  hizo huku Laura akimshitaki mwanamziki huyo kwa makosa matatu ikiwemo uzembe, kumsababishia athari, mawazo na kupelekea kuzorota kwa afya yake pamoja na kosa la udanganyifu

Mtandao wa whatsApp kuanza kurusha matangazo
Wanafunzi wa kike wawadhibiti wanaume waliovamia bweni lao usiku

Comments

comments