Usambazaji wa gesi majumbani katika jiji la Dar es Salaam unaanza kesho Jumanne, Aprili 24 huku bei ya gesi ikipungua kwa asilimia 40 ya bei ya sasa kwenye mitungi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medadi Kalemani wakati akijibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika utaratibu wa mawaziri waliojiwekea.

Amesema kiuwa gharama za kuunganisha gesi kwa wateja watakaopitiwa na bomba hilo itakuwa Sh 200,000 hadi 1 milioni kutegemeana na umbali kutoka lilipo bomba kuu.

Hata hivyo ametaja baadhi ya maeneo yatakayoanza kunufaika kuanzia kesho ni Ubungo, Mwenge, Kijitonyama, Gongolamboto, Shekilango na Mikocheni na kazi hiyo itadumu kwa miezi miwili.

 

Video: Maadhimisho siku ya malaria duniani kufanyika kitaifa Kasulu
JPM- Nitaendelea kuchapa kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania