Wabunge wa upinzani nchini Zimbabwe wametoka nje ya bunge mara baada ya Rais wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa kuanza kuhutubia Bunge la nchi hiyo.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa hatua hiyo ni ishara ya hasira ya wabunge hao baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais na wabunge wa mwezi Julai mwaka huu.

Aidha, wanachama wa ‘Movement for Democratic Change’ ( MDC) wakiongozwa na kiongozi wao, Nelson Chamisa ambaye alishindwa na Mnangagwa kwenye uchaguzi huo, walianza kupiga kelele katika bunge na baadaye kuondoka muda mfupi baada ya Mnangagwa kuanza kusoma hotuba yake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baadaye wabunge hao walianza kuimba nyimbo za kukikashifu chama kinachotawala cha Zanu PF.

Hata hivyo, kwenye hotuba yake Rais Mnangagwa amesisitiza kwamba suala la uchaguzi wa mwezi Julai ni historia, na kwamba sasa ni wakati wa wanasiasa kutekeleza ahadi walizozitoa kwa wapiga kura.

LIVE: DC Jokate anaongea na waandishi wa habari muda huu. Tazama
Video: Lissu tumepigwa, CCM yamshangaa RC Makonda