Kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Pyramids FC nchini Misri makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wamejiandaa vizuri.

Mwakalebela ambaye tayari yupo nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya kuipokea timu, ameeleza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na watapambana kupata matokeo.

Amesema wana matumaini ya ushindi baada ya kugundua kuwa huko Misri Pyramds inazungumziwa kama timu ya kawaida suala ambalo amelisema linawapa nguvu.

“Unajua hapa Misri Pyramids wanaisema kuwa ni timu ya kawaida kabisa, hivyo inatupa nguvu kuelekea mechi ya marudiano, naimani tutafanya vizuri ikiwemo kupindua matokeo,” amesema Mwakalebela

Kauli hiyo imekuja ambapo hivi sasa Yanga tayari wameshatua Misri kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itakuwa ya kupindua matokeo kufuatia kupoteza kwa mabao 2-1 hapa nyumbani.

Mtoto aishi miaka 12 na jiwe puani
Mlevi aliyemtishia polisi paka atupwa jela miaka 5

Comments

comments