Kuamua kuwa unahitaji kubadilisha kazi yako si jambo linalokujia usiku mmoja tu, mara nyingi hufanyiwa maamuzi baada ya muda fulani.

Kamwe usiamue kuacha kazi kwa sababu ya hisia zako tu, kwa mfano, kuamua kuacha kazi kwa sababu ya ugomvi wa siku moja kazini inachotakiwa kufanya ni kukaa na kuchukua muda kuamua ni wakati gani unaofaa kuacha kazi yako kabla ya kufanya maamuzi, haya ni baadhi ya mambo ya kukusaidia kuamua wakati sahihi wa kubadilisha kazi yako.

1. Kazi yako inakuchosha sana

Kazi unayofanya imekuwa ya kawaida sana na haikupi changamoto mpya? Hakuna tena hamasa na msisimko wa kufanya kazi? mara zote unawaweza kuomba kuongezewa au kubadilishiwa kazi, lakini kama unaona hili halitatokea karibuni, basi ni wakati wa kutafuta na fursa za kusisimua na zenye changamoto zaidi, hata hivyo kuwa makini hapa, pima mawazo yako vyema unaweza kwenda kwenye kazi nyingine na ukakuta inachosha vile vile.

2. Kazi zinakuzidi Kupita Kiasi

Shinikizo la kazi linapokuwa kubwa kuzidi uwezo wako linaweza kukusababishia matatizo ya afya kwa muda mrefu, unaweza kujitahidi kufanya mzigo mkubwa wa kazi kwa muda mfupi mwanzoni, lakini ikiwa ni kazi kubwa na kwa muda mrefu huku malipo yakiwa duni, mara nyingi inavunja moyo na huenda ikawa ni wakati mzuri wa kubadili kazi yako.

3. Kuwa na mazingira duni ya kazi

Ikiwa kumefanyika mabadiliko katika mfumo wa kazi unaobadilisha mazingira au utamaduni kukuathiri kwa njia mbaya, tafuta namna ya kufanya mabadiliko, ikiwa hakuna kinachoweza kufanyika ni vyema uanze kuangalia nafasi nzuri zaidi hasa kama hali ya sasa inathiri ustawi wako.

4. Kuwa na maendeleo kidogo ya kazi

Wakati mwingine unaweza kupandishwa cheo hadi kufikia mwisho katika kampuni ambayo ni ndogo sana kwa maendeleo zaidi ya hapo, ikiwa unajisikia kama kazi yako imefikia kikomo, na haiwezi kuendelea zaidi ya hapo basi ni bora kuanza kuangalia fursa ya kuendeleza kazi yako katika shirika lingine au kampuni kubwa zaidi.

5. Migogoro ya mshahara

Wakati mwingine unaweza kujisikia kama unastahili kulipwa zaidi kwa sababu ya kiasi cha kazi unachofanya na ubora wa kazi unaotoa au unaweza kujiona kuwa unaweza kupata kazi inayolipa vizuri zaidi vyovyote tu, hamu ya kupata mshahara mkubwa zaidi inaeleweka kabisa ikiwa mwajiri wako wa sasa hayuko tayari kuongeza mshahara na hivyo unapaswa kuzingatia kutafuta mwajiri mwingine.

6. Kutokuwa na mahusiano mazuri na meneja wako

Kama hupatani na bosi wako vizuri basi kufikiria kwenda kazini kila siku inaweza kukupa msongo wa mawazo sana, jaribu kutafuta suluhu na bosi wako ili muweze kuelewana, ikiwa haiwezekani hakuna haja ya kuwa na ‘stress’ kila wakati unapomwona bosi wako. Fikiria namna ya kutafuta mtazamo mwingine wa ajira yako.

Wakati wa kufikiria kuacha kazi yako ya sasa, mara zote anza kwa kupima kama hali inaweza kurekebishwa kwa namna yoyote, Je, kuna kitu wewe au bosi wako anaweza kufanya ili kubadilisha hali hiyo? Ikiwa njia inaweza kupatikana, basi fanyia kazi hilo kwanza. Sio vyema kuwa aina ya mtu ambaye anakimbia kila sehem akikutana na tatizo dogo tu. Ikiwa hakuna chochote kinachoweza kufanyika, huu unaweza kuwa wakati wa kutafuta fursa bora zaidi. Jaribu kutafuta fursa katika mtandao kama BrighterMonday.

Zitto Kabwe aachiwa kwa dhamana
Majaliwa awahakikishia wanakijiji kupata huduma safi ya maji

Comments

comments