Umoja wa Mataifa (UN) umetuma misaada ya dharura nchini Somalia kufuatia mvua kubwa ambazo zinaendelea  katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo na kusababisha mafuriko.

Misaada hiyo imetumwa hasa katika Wilaya ya Beletweyne ambapo taarifa zinasema watu zaidi ya 270,000 wameachwa bila makazi baada ya nyumba zao kuharibika katika mafuriko.

Tayari helikopta imetumwa kusaidia shughuli za kibinadamu kati ya Beletweyne na sehemu zilizo karibu zilizoathiriwa vibaya na mafuriko kutoka Mto Shabelle ikiwemo familia 4,000 kutoka vijiji saba kwenye Wilaya ya Beletweyne.

Mvua kubwa na mafuriko yameendelea kuzikumba Somalia, Sudan Kusini na Kenya mwaka huu na Watabiri wa Hali ya Hewa wanatarajia mvua hizo kubwa zitaendelea kunyesha hadi Disemba.

CAG Kichere akabidhiwa ofisi na Assad "nitalinda kwa wivu", afunguka mahusiano na Bunge
Maandamano ya Wanahabari Uganda yatawanywa na mabomu