Wafanyakazi wote wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa wametakiwa kufanya kazi zao wakiwa majumbani kwa takribani wiki tatu kutokana na mripuko wa virusi vya Corona.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mpango huo una lengo la kupunguza wingi wao katika ofisi hizo wakati wakiendelea kufanikisha majukumu yao.

Mapema wiki hii mwanadiplomasia mmoja wa Kifilipino wa ofisi hizo za Umoja wa Mataifa aligundulika kuwa na virusi vya corona.

Mashirika mengi na makampuni duniani kote, likiwemo Shirika la Fedha Duniani IMF, yamerudisha wafanyakazi wao majumbani kwa lengo la kupunguza usambaaji wa virusi hivyo.

CORONA: Ikulu ya Marekani yatikiswa, Trump apimwa, majibu yatangazwa
Polisi wazungumzia taarifa za Mdee, Bulaya kupigwa

Comments

comments