Leo June 14, 2018 ni siku ya maadhimisho ya utoaji damu duniani ambapo siku hii imelenga kutoa shukrani kwa watu wote waliojitokeza kutoa damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wagonjwa waliopungukiwa na damu na walio hatarini kupoteza maisha kwa kukosa damu.

Siku hii ya leo Shirika la Afya duniani (WHO), na Taasisi za zimelenga kutoa uelewa kwa watu juu ya umuhimu wa watu kujitolea damu mara kwa mara ili kuhakikisha upatikanaji wa damu safi na salama pamoja na vifaa vyake kwa ajili ya wagonjwa duniani kote.

Utoaji wa damu unasaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka kwani wagonjwa wanaougua na kuhatarisha maisha huokolewa na damu ambazo zipo katika benki ya kutunza Damu hasa wale wagonjwa wa dharula na wale wanaofanyiwa upasuaji wakiwemo wamama wanaotoka kujifungua.

Nchi nyingi zinakumbana na tatizo la upungufu wa damu katika benki za damu na tatizo la kupata damu safi na salama na ndio maana siku kuna haja wa watu kutambua juu ya umuhimu wa kuchangia damu safi na salama kwa ajili ya watu wengine waliopo mahospitalini wanaoteseka na tatizo la upungufu wa damu mwilini.

Mwaka huu maudhui ya siku hii ni kuhamasisha utoaji damu kama kitendo cha ushujaa, uzalendo na utu.

Hivyo wamekuja na kauli mbiu inayosema ”be there for someone else. Give blood. share life” yaani fanya uwepo wako kwa mtu mwingine, gawa sehemu ya maisha yako kwa mtu mwingine kwa kumtolea damu. Lengo likiwa kujenga utayari kwa watu katika suala zima la utoaji damu kwa hiari na kuhamasisha watu kujali watu wengine na kuguswa na maisha ya watu hasa wale waliokubwa na majanga.

Hivyo basi katika siku hii ya utoaji damu duniani watu wote waguswe na suala hili na kujitolea kutoa damu kwa ajili ya kuwasaidia ndugu jamaa na marafiki watakaokumbwa na shida ya upungufu wa damu kutokana na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wao.

Martial kukimbia benchi Manchester United
Video: 'Sinema' ya Lembeli akirudi CCM, Vigogo 6 Bodi ya Mikopo Kitanzini