Waziri wa afya, Ummy Mwalimu amesema kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuelezea umma kuwa mtoto wa Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe  ameathirika na virusi vya Corona kimekiuka utaratibu wa kitabibu.

Amesema kuwa Makonda amekiuka taratibu za kitabibu ambazo zinaeleza kuwapo kwa usiri wa taarifa za ugonjwa kati ya mgonjwa na daktari ambapo amesema katika taarifa ambazo amekuwwa akizitoa kuhusu idadi ya wagonjwa waliothibitika nchini kuwa na maambukizi ya virusi vya corona huzitaja kwa idadi,jinsi, umri na eneo wanakotoka na si kwa majina kama alivyofanya Makonda.

Ikumbukwe machi 24 mwaka huu Makonda akiwa katika ukaguzi wa maeneo ya mkoa wake katika kukabiliana na Corona alisema anataarifa kuwa mtoto mmoja ambaye hakumtaja jina wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anamaambukizwa ya virusi vya Corona.

Akipinga kitendo hicho cha Makonda ,Waziri Ummy amesema mkuu huyo alimkosea Mbowe kwani hata kufahamika kwa jina la Isabella Mwampamba (49) na kutajwa kama mgonjwa wa kwanza kuugua Corona nchini kulitokana na mgonjwa mwenyewe kujitaja.

”Ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari mimi kama waziri mwenye dhamana sijawahi kutaja jina, Isabella alitajwa na baadhi ya watu na mwenyewe akajitaja pia mwana FA alijitaja mwenyewe kuna taratibu zinatuzuia kutaja majina” amesema Ummy

Ameeeleza kuwa taarifa ambazo zinatakiwa kuaminiwa ni kutoka kwa Waziri Mkuu, Msemaji mkuu wa serikali Wizara ya Afya Tanzania bara na Zanzibar kama ilivyoelekezwa na Rais John Magufuli  hivi karibuni.

Marekani yaongoza idadi ya waathirika wa Corona Duniani
Mgonjwa wa Corona aliyefariki kenya alikuwa na Kisukari

Comments

comments