Wizara ya Uvuvi na Ufugaji kwa kushirikiana na (Tamisemi) wamewaagiza wakurugenzi, watendaji wa mitaa na wakuu wa wilaya zote nchini kuacha mara moja kufungia minada ya samaki ya ng’ombe kwa kisingizio cha ugonjwa wa covid 19.

Akizungumza alipotembelea soko la samaki la Feri na mnada wa ng’ombe Pugu, Naibu waziri wa mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega amesema kuwa msimamo wa serikali upo pale pale haujazuia biashara yoyote ikiwemo minada ya samaki na ng’ombe.

Alipokuwa Feri alisema ” Samaki ndio chakula cheye kirutubisho cha Omega3, ambayo inasaidia kupambana na maradhi. Endeleeni kuchapa kazi lakini mchukue tahadhari”

Ulenga ametoa agizo hilo baada ya kile kinachoelezwa kuwa tayari kuna taarifa za masoko ya minada kufungwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Ngala Nzega na Chumbi Muhoro, ambapo wafugaji wamelalamika kufukuzwa na kupoteza baadhi ya mifugo yao.

Maajabu ya karafuu katika mwili wa binadamu
Corona: Italia, Uhispania wamepoteza watu zaidi ya 800 kwa kila nchi jana