Msemaji wa Umoja wa Ulaya, Marta Wieczorek amesema halmashauri Kuu ya umoja huo inaamini uchumi wa Ulaya utaingia katika mdororo mwaka huu kutokana na athari za mlipuko wa Virusi vya Corona.

Hata hivyo, amesema bado hakuna data rasmi za makadirio hayo, lakini ipo hali kubwa ya sintofahamu juu ya madhara ya janga hilo.

Awali, Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na soko la ndani, Thierry Breton alisema wakuu wa umoja huo wanatabiri kuwa mdororo huo wa kiuchumi utakuwa katika kiwango cha asilimia moja.

Aidha, Breton amekiambia kituo cha televisheni cha BFMTV kuwa kabla ya mlipuko wa Virusi vya Corona, Umoja wa Ulaya ulitazamia uchumi wake kukua kwa asilimia 1.4.

Kesi ya Zitto Kabwe kuanza kuunguruma kisutu leo
Mwanamke awa wakwanza kujitolea jaribio chanjo ya Corona

Comments

comments