Waziri mkuu wa Ukraine, Oleksiy Honcharuk leo amesema kuwa amewasilisha barua yake ya kujizulu kwa Rais Volodymyr Zelensky, kufuatia ripoti za kurikodiwa akitoa matamshi ya matusi dhidi ya Rais huyo.

Honcharuk amesema hatua yake ya kujiuzulu imenuwia kuondoa shaka juu ya heshima na utiifu alionao kwa Rais.

Awali vyombo vya habari vya Ukraine viliripoti juu ya sauti iliyorekodiwa ambapo Honcharuk anadaiwa kumuelezea Rais Zelensky kama mtu mwenye ufahamu wa kale kuhusu masuala ya kiuchumi na uwezo mdogo wa kujifunza kuhusu nyanja hiyo.

Hadi sasa bado haijabainika wazi iwapo Honcharuk ambaye licha ya kuwa mwanasiasa pia ni mwanasheria alieunga mkono mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini humo ataacha kweli nafasi hiyo ambapo Bunge litapaswa kuidhinisha barua yake ya kujiuzulu.

Marekani yakiri wanajeshi wake kufikiwa na makombora ya Iran
Wanandoa wauawa kwa kucharangwa mapanga na ndugu