Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ametoa hamasha kwa wakazi Kisiwa cha Ukerewe kilichopo mkoani Mwanza kutambua umuhimu wa kufuga nyuki na faida ya asali kiuchumi na kiafya.

Ametoa ruhusa  kwa wananchi wenye nia ya kufuga nyuki kuitumia misitu ya Hifadhi mitano iliyopo katika Kisiwa hicho  inayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya hiyo kutundika mizinga yao katika misitu hiyo.

Mbeya: Madiwani 11 wa Chadema wajiunga CCM

Kanyasu amesema lengo ni kuwasaidia wananchi kubadili mfumo wa maisha kwa kuanza  kufuga nyuki kibiashara  badala ya  kulima na kuvua samaki pekee.

Akizungumza na Kikundi cha Walemavu wanaojishughulisha na useremala wa kutengeneza mizinga ya nyuki ya kisasa mjini Nansio Ukerewe, amesema  misitu hiyo mitano yenye jumla ya zaidi ya  hekta 1300 itawasaidia  kuitumia kufuga nyuki kibiashara.

Amesema kutokana na ongezeko kubwa la watu wapatao zaidi 400,000 katika Kisiwa hicho chenye ukubwa usiozidi kilomita za mraba 700 ambalo ni eneo  la nchi kavu , Wakazi wa Kisiwa hicho wana kila sababu ya kujiingiza kufuga nyuki.

Kabendera aachiwa huru, faini milioni 400

Amewahakikishia uwepo wa soko la uhakika kutokana na mahitaji makubwa ya asali katika nchi ya China na Marekani, amesema hata hivyo Tanzania bado haijaweza kukidhi mahitaji ya soko hilo.

Amesema China pekee inahitaji asali tani 600,000 kutokana na uzalishaji duni Tanzania bado haijaweza  kusafirisha hata nusu tani ya  asali hiyo inayohitajika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa wilaya  Halmashauri hiyo, Esther Chaula ameahidi kutoa mkopo kwa kikundi hicho cha Walemavu ili waweze kutengeneza mizinga mingi itakayorahisisha upatikaji wa mizinga ya kutosha kwa ajili ya kufugia nyuki.

Togo: Faure ashinda kwa kishindo urais
Mbeya: Madiwani 11 wa Chadema wajiunga CCM