Vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa vimemshukia mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kwa madai ya kutumia kauli mbiu ya vyama hivyo katika kampeni zake.

Akiongea katika mkutano wa kampeni za za kumnadi mgombea urais anaungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema kuwa kitendo cha Dk Magufuli kuanza kutumia kauli mbiu za umoja huo kinaonesha jinsi alivyoshindwa kupambana na upinzani dhidi yake.

“Magufuli anasema hakuna mtu anayeweza kuwatisha, lakini atambue CCM yake maji yameanza kuingilia kwenye pua sasa wanashika popote na kutapatapa,” alisema. “Ndio maana unasikia anasema Movement For Change yaani M4C ni Magufuli For Change, hawana haya kweli wameishiwa hoja, hivi M4C NA Magufuli ilianza ipi?” aliwahoji wananchi walioitikia kwa sauti ya juu ‘M4C’.

Sumaye aliongeza kuwa hali hiyo ni dalili tosha kuwa baada ya CCM kuiongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50, hivi sasa fikra na mawazo ya chama hicho imefikia kikomo na kinapaswa kupumzishwa.

Hayo yanafuatia kauli ya Dk Magufuli alipokuwa mkoani Kigoma hivi karibuni ambao aloiwaambia wananchi kuwa maana ya ‘M4C’ inayotumiwa na Chadema ni ‘Magufuli For Change.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa ‘M4C’ ilianza kutumiwa na Chadema mwaka 2006 kama kampeni maalum ya kuongeza hamasa ya kufanya mabadiliko katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Magufuli Awaonya Wakimbizi Wanaoingia Na Silaha Nchini
Tanzania Yaambulia Patupu All African Games