Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia katika mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Amesema hayo wakati akilihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni, Merkel amewataka wananchi kutambua jukumu lao katika kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo.

Katika hotuba hiyo ya aina yake na isiyo ya kawaida aliyoitoa Jumatano jioni, Merkel aliwasihi wananchi kuendelea kufuata maagizo yaliyotolewa na serikali ya kubakia majumbani ambapo  ametoa wito kwa taifa kuungana pamoja.

Kwa mujibu wa kitu cha habari cha  DW, Hotuba hiyo ameitoa siku moja baada ya Ujerumani kutangaza hatua mpya na madhubuti za kupunguza kuenea kwa virusi hivyo.

Siku ya Jumatano Ujerumani ilirekodi ongezeko la zaidi ya visa 1,000 vya virusi vya corona ikilinganishwa na siku moja iliyopita.

Kwa mujibu wa kituo cha utafiti cha John Hopkins, watu 12,300 wameambukizwa virusi hivyo nchini Ujerumani na wengine 28 wamekufa, huku zaidi ya watu 100 wakiwa wamepona.

Hata hivyo, Ujerumani imeifunga mipaka yake kwa raia wasiotoka kwenye nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, imezuia safari na imeamuru kusimamishwa kwa shughuli nyingi za umma, kufungwa shule pamoja na biashara.

Ikumbwe siku ya Jumatano Italia iliripoti karibu vifo 500 vya virusi vya corona, idadi kubwa kabisa ya vifo kwa siku moja ambayo haijawahi kushuhudiwa katika taifa lolote lile duniani tangu kuzuka kwa virusi hivyo nchini China Desemba mwaka uliopita.

Noti ya Tanzania haibebi vimelea vya Virusi
Makamu wa Rais wa Pili wa bunge la Burkina Faso afariki kwa Corona

Comments

comments