Wanajeshi wa Uhispania waliopelekwa kupambana na virusi vya Corona wamebaini wagonjwa wazee waliotelekezwa na wengine wamekufa kwenye makaazi ya wazee.

waziri wa ulinzi wa Uhispania Margarita Robles wakati wa mahojiano na kituo binafsi cha televisheni cha Telecinco amesema kuwa jeshi wakati wa utekelezaji majukumu waliyopewa wamewakuta baadhi ya wazee wakiwa wametelekezwa na wengine wakiwa wamekufa kwenye vitanda vyao.

Wakati hayo yanajiri, vifo vilivyotokana na virusi vya Corona nchini Uhispani vimepanda kwa kasi na kufikia watu 2,182 siku ya Jumatatu baada ya watu 462 kufariki dunia katika muda wa saa 24.

Wakati huo huo, uwanja wa ndani wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu uitwao Palacio de Hielo uliopo kati kati ya mji mkuu Madrid umegeuzwa kuwa chumba cha muda cha kuhifadhi maiti.

Chini ya miongozo ya kupambana na virusi vya Corona, wafanyakazi wa afya wanatakiwa kuiacha miili ya watu walioshukiwa kufa kwa ugonjwa wa COVID-19 hadi pale daktari atakapowasili. Lakini kutokana na wimbi la vifo vinavyoendelea muda wa kusubiri unaweza kuwa mrefu zaidi.

Mara: Wahamiaji haramu wakutwa na vitambulisho vya taifa
Saliboko ajiwekea malengo Lipuli FC

Comments

comments