Vyombo vya dola nchini Indonesia vinamshikilia raia wa Tanzania, Abdul Rahman Asman baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuingiza dawa za kulevya nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, Asman alikamatwa Januari 30 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Bali. Baada ya kumfanyia upekuzi na vipimo vya CT Scan pamoja na X-Ray, walibaini kuwa alikuwa na pakiti za plastiki zenye unga ndani ya tumbo lake.

“Mtanzania huyo alikamatwa Bali akiwa na kilo kadhaa za dawa za kulevya,” AFP inakikariri chanzo chake cha habari ingawa hakikueleza aina ya dawa hizo.

Indonesia inatajwa kuwa moja kati ya nchi zenye sheria kali za kuzuia na kupambana na dawa za kulevya na hutoa adhabu hadi ya kifo kwa mtu anayekutwa na hatia.

Hadi sasa, wapo watuhumiwa kadhaa wakiwemo raia wa Uingereza, Marekani na Afrika Magharibi waliohukumiwa kifo baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Rais wa Indonesia, Joko Widodo amevipa mamlaka makubwa vyombo vya ulinzi na usalama katika kupambana na dawa za kulevya. Askari wanaruhusiwa kuwaua wafanyabiashara wa dawa za kulevya endapo watakuwa wabishi wakati wa ukamataji.

Bilionea wa dawa za kulevya ‘El Chapo’ akutwa na hatia
Solskjaer afunguka baada ya kupigwa na PSG nyumbani