Sheria mpya imepitishwa Nchini Uganda inayowabana wanaosaidia ombaomba mtaani, ambapo wananchi watakaowapa fedha au chakula watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuomba mitaani katika Jiji la Kampala watafungwa jela miezi sita au kulipa faini ya Dola za Marekani 11.

Meya wa Jiji la Kampala, Elias Lukwago amesema lengo la sheria hiyo ni kukomesha biashara ya usafirishaji watoto na unyanyasaji wa vitendo vya ngono kwa watoto.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Meya huyo imeeleza kuwa Serikali inakadiria kuwa watoto wenye umri wa miaka saba hadi 17 takribani 15,000 wanaishi katika mitaa mbalimbali katika Jiji hilo.

Inaelezwa kuwa watoto wengi wamekuwa wakisafirishwa kutoka vijijini na kupelekwa mijini wanapoishi kwenye chumba kidogo na sheria hiyo imezuia kupanga nyumba kwa ajili ya biashara za ngono au kutumia watoto kufanya biashara.

Lukwago amesema sheria inawalenga wazazi na mawakala wanaowatumia watoto kupata fedha pamoja na wazazi wanaowatumia kuuza vitu au kuomba mitaani ambao nao watapewa adhabu.

“Biashara hii inafaida kubwa kwa wale wanaowatumia watoto kutoka sehemu mbalimbali Nchini Uganda na kuwalea katika mitaa ya Kampala, ni biashara hivyo tunataka kuimaliza” ameongeza Meya Lukwago

Aidha amesema pia sheria hiyo itasaidia kudhibiti biashara ya uingizaji wa ombaomba kutoka Nchi jirani na wanawake wanaofika na watoto wao kuomba mitaani.

Hatahivyo, baadhi ya raia wa Uganda hawajakubaliana na mikakati hiyo kwa madai kuwa inabagua raia wa Uganda hasa wa tabaka la chini.

 

 

Mtuhumiwa wa tukio la utekaji wa 'Mo Dewji' afikishwa Mahakamani
Afa kwenye ndege baada ya kumeza kete 246 za 'Unga'