Siku chache baada ya rais wa Uganda, Yoweri Museveni kusitisha huduma za usafiri wa Umma zikiwepo bodaboda ili kuzuia maambukizi ya virusi vya covid 19, watu wawili waliokuwa wakienda kazini kwa kutumia bodaboda wamepigwa risasi na Polisi.

Wawili hao, Alex Olyem na Kasim Ssebude wanapatiwa matibabu Hospitali, walipigwa risasi hizo wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki barabara ya Goma.

kwamujibu wa gazeti la Daily Monitor  la nchini Uganda, Olympics alipigwa risasi mguuni na Ssebude alipigwa tumboni, Wametuhumiwa na Polisi kwa kukiuka maagizo ya rais Museveni.

Akizungumzia tukio hilo, Olyem amesema hakuangalia taarifa ya habari siku rais alipotangaza hatua zinazochukuliwa kudhibiti virusi vya Corona hivyo hakujua kama bodaboda zimepigwa marufuku.

Gazeti Hilo limeripoti kuwa, wakati wanaelekea kazini walizuiwa na Polisi walipojaribu kuuliza kosa walilofanya risasi mbili zilifyatuliwa hewani na baada ya hapo, Polisi wakaanza kuwapiga risasi.

Hata hivyo, Msemaji wa Polisi Patrick Onyango, amedai wawili hao walipigwa risasi baada ya kujaribu kumshambulia Afisa wa Polisi.

Afrika kusini: Wawili wafa maambukizi yafika 1000 virusi vya Corona
Marekani yaongoza idadi ya waathirika wa Corona Duniani