Padri Elio Zanei wa kanisa katoliki Parokia ya Angal nchini Uganda amejichimbia kaburi lake mwenyewe ili kujiandaa na kifo chake baada ya kupokea taarifa ya vifo vya nduguzake wengi kwa ugonjwa wa virusi vya Corona.

Padri Zanei ambaye ameishi parokia ya Angal nchini Uganda kuanzaia mwaka 1996 akihudumia watu wa kanisa hilo, amewashangaza waumini wake alipochimba kaburi hilo wakati akiomboleza vifo hivyo vya ndugu zake.

“Nimepoteza ndugu zangu, marafiki na waitalia wenzagu kwa virusi vya Corona. ni hali ya kutisha kuona watu wetu wanakufa Italia. nawasihi wakristo wenzangu kujiandaa kwa siku za mwisho kwa maombi na kujifunza jinsi ya kusameheana” Amesema padri huyo .

Pia ameacha maelekezo kuwa atakapokufa asirudishwe italia nchini kwao, azikwe kwenyekaburi hilo, huku ikielezwa kuwa tokea ameanza kupokea habari za vifo Italia amekuwa akiishi kwa kujitenga.

Gazeti la Daily Monitor la nchini humo limesema licha ya padri huyo kuchimba kaburi pia ameagiza kununuliwa jeneza lake kabisa.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Nebbi, Christopher Omara amewaomba viongozi wengine wa dini kumfariji padri huyo kwa wakati mgumu anaopitia.

Mpaka sasa, jumla ya watu 9,134 wamefariki kwa virusi vya corona ndani ya nchi ya Italia pekee yake, Serikali ya Italia imeamuru kufungwa kwa kila kitu na watu kutakiwa kukaa ndani ya nyumba zao. Kuna wasiwasi kuwa zuio hili huenda likazidi tarehe 4 mwezi Aprili, 2020.

Membe: ''Tusipuuzie Corona tutaumwa na wengine tutakufa''
Video: LIPUMBA amjibu CAG upotevu wa milioni 300 CUF, Akili kuzihamisha