Nchini Uganda kiongozi wa Upinzani, Dkt. Kizza Besigye kupitia Chama cha Forum for Democratic Change (FDC) amekataa ombi la kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao, baada ya kuwania nafasi ya Urais mara 4 tangu mwaka 2001.

Uamuzi huo umekiacha njiapanda Chama hicho ambacho kinafanya harakati za kumtafuta Mgombea wa Urais katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema 2021.

Msumbuji yapokea uenyekiti wa Baraza la mawaziri SADC

FDC imeahirisha uteuzi wa wagombea Urais mara mbili wakiwa na matumaini Dkt. Besigye ambaye ni Kiongozi wa Chama hicho angebadili msimamo wake na kuchukua fomu za uteuzi

Uganda Chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) ndio kipo madarakani tangu mwaka 1986 kupitia kwa Rais Yoweri Museveni.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 14, 2020
Wiki mbili za Waziri Mkuu kwa RC,DC na Mkurugenzi mtendaji