Kimbunga kimeikumba Ufilipino, mtu mmoja amefariki na kimeleta mvua nyingi ambayo imesababisha kusitishwa kwa safari za anga na ofisi za serikali kufungungwa katika mji mkuu Manila.

Serikali za mitaa zimewaondoa watu 225,000 kutoka maeneo hatari kabla ya kuwasili kwa kimbunga Kammuri kunachotarajiwa usiku wa leo, kinachofahamika nchini humo kama Tisoy.

Kimbunga Kammuri, ni cha cha 20 kupita katika nchi hiyo mwaka huu, kimesababisha upepo unaovuma kwa kasi ya kilometa 150 kwa saa, na kuharibu baadhi ya nyumba na majengo na kuangusha miti katika maeneo ya miji.

Hadi sasa  tahadhari ya mafuriko, ongezeko la dhoruba na maporomoko ya ardhi vimeendelea kutolewa nchini humo huku mtu mwenye umri wa miaka 33 akifariki baada ya kushika umeme wakati akijaribu kutengeneza paa la nyumba yake.

DRC: Jeshi laua waasi 80 wa ADF
DC kigamboni atangaza vita watoto kukaa 'vibanda umiza'

Comments

comments