Mabingwa wa dunia timu ya taifa ya Ufaransa imetangazwa kuwa kinara kwenye orodha ya viwango vya ubora wa soka ambavyo hutolewa kila mwezi na la soka la kimataifa FIFA.

FIFA wametoa orodha hiyo kwa mara ya kwanza, tangu fainali za kombe la dunia zilipomalizika nchini Urusi, na taifa hilo la barani Ulaya kutwaa ubingwa, baada ya kuibanjua Croatia mabao 4 kwa 2 mjini Moscow Julai 15.

Ufaransa wamepanda kwa nafasi sita wakitoka nafasi ya saba, huku mabingwa wa dunia mwaka 2014 Ujerumani wakitupwa hadi katika nafasi ya 15.

Ufaransa wanafuatiwa na Ubelgiji waliokamata nafasi ya pili kwenye orodha hiyo, huku Brazil wakishuka kwa nafasi moja na kuwa namba tatu duniani, wakifuatiwa na Croatia waliofika fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya fainali za kombe la dunia.

Mwezi uliopita Croatia walikua katika nafasi ya 20, hivyo wamepanda kwa kiwango kikubwa katika historia ya soka lao kwa nafasi 16.

Uruguay iliyofika hatua ya robo fainali imepanda hadi kwenye nafasi ya tano ikitoka nafasi ya tisa, huku England waliomaliza katika nafasi ya nne wakiwa katika nafasi ya sita.

Argentina wameporomoka kwa nafasi 6 katika orodha hiyo ya viwango vya ubora wa soka kwa mwezi Agosti na kushika nafasi ya 11, huku wenyeji wa fainali za kombe la dunia 2018 Urusi waliokua katika nafasi ya 71 kabla ya kuanza kwa fainali hizo, wamepanda kwa nafasi 21 na kuwa katika nafasi ya 49.

Kwa upande wa Tanzania imeendelea kushika nafasi ya 140.

Ifuatayo ni orodha ya nchi zilizoshika nafasi ya kwanza hadi ya 30 kwa mwezi Agosti.

  1. Ufaransa 2. Ubelgiji 3. Brazil 4. Croatia 5. Uruguay 6. England 7.Ureno 8. Uswiz 9. Hispania 10. Denmark 11. Argentina 12. Chile 13. Sweden  14. Colombia 15. Ujerumani 16. Mexico 17. Uholanzi 18. Poland  19. Wales  20. Peru  21. Italy 22. Marekani  23. Austria 24. Tunisia 25. Senegal  26. Slovakia 27. Ireland Ya Kaskazini       28. Romania 29. Jamuhuri Ya Ireland  30. Paraguay

 

Casemiro ataka ushindi wa Atletico Madrid uheshimiwe
Video: Walimpiga kwasababu alifanya fujo- IGP Sirro