Shirikisho la soka barai Ulaya UEFA limemthibitisha Aleksander Ceferin kuwa mrithi wa Michel Platin ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa kujihusisha na kandanda kwa muda wa miaka sita.

Ceferin ambaye ni raia wa nchini Slovakia, ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya urais wa UEFA kwa kupata kura 42 huku mpinzani wake Michael van Praag akipata 29.

“Ni jambo la heshima sana kupewa nafasi ya kuwa Raisi wa UEFA na kupewa majukumu makubwa katika soka. Inamaana kubwa sana kwangu” amesema Ceferin.

Mara baada ya kushinda katika uchaguzi huo, Ceferin ataliongoza shirikisho la soka barani Ulaya UEFA hadi mwaka 2019 pale uchaguzi mkuu utakapoitishwa.

Waziri Mkuu azindua miongozo ya Mfumo wa Anwani za Makazi
Wagner Ribeiro: Neymar Amekataa Mshahara Wa Pauni 650,000