Uchaguzi ulioahirishwa kwa wiki moja nchini Nigeria, unatarajia kufanyika hii leo Jumamosi, lakini baadhi ya watu wanahofu kubwa ya kujitokeza kwenye vituo vya kupigia kura kufuatia vitisho vya kushambuliwa na kundi la Boko Haram.

Rais Muhammadu Buhari amewataka wananchi wa Nigeria wajitokeze kwa wingi kweda vituoni kupiga kura leo Jumamosi na ameahidi kwamba usalama umeimarishwa katika maeneo yote ya nchi hiyo.

Katika uchaguzi huo ulioahirishwa wiki iliyopita Rais Buhari anapambana vikali na mfanyabiashara, Atiku Abubakar ambaye hapo awali alikuwa makamu wa Rais.

Aidha, tume huru ya uchaguzi nchini Nigeria wiki iliyopita iliahirisha uchaguzi huo wakati Wanigeria zaidi ya milioni 72 walipokuwa wanajitayarisha kwenda kupiga kura katika vituo mbalimbali nchini humo.

Akihutubia taifa kwenye televisheni Rais Buhari amewataka Wanigeria wasiwe na wasiwasi na wawe na imani kwamba tume ya uchaguzi itatimiza jukumu lake, huku mpinzani wake kiongozi wa chama kikuu cha upinzani PDP, Atiku Abubakar ametoa wito huo huo kwa wapiga kura.

Zaidi ya Wanigeria milioni 84 wameandikishwa kupiga kura kwenye taifa hilo lenye wakaazi milioni 190 la Magharibi mwa Afrika.

 

 

Mbivu mbichi za Maalim Seif, Prof. Lipumba machi 17, Katakata ya umeme yaanza
R Kelly akabiliwa na kifungo cha miaka 70 jela, ajisalimisha polisi