Tume huru ya uchaguzi nchini Nigeria (INEC) imeahirisha uchaguzi wa rais na wabunge kwa muda wa wiki moja, muda mfupi kabla ya vituo vya uchaguzi kufunguliwa.

Mwenyekiti wa INEC, Mahmood Yakubu amesema kuwa wamechukua uamuzi huo mgumu wa kuahirisha uchaguzi ili kuweza kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa mafanikio makubwa katika vituo vyote.

Aidha, ametoa maelezo mafupi kuhusu uchaguzi huo ambao ulitarajiwa kufanyika hii leo siku ya Jumamosi lakini kasema haitawezekana kuendelea tena na uchaguzi huo mpaka pale muda uliopangwa utakapofika.

Hata hivyo, Vyombo vya habari vya ndani nchini Nigeria vimeripoti kuwa vifaa vya kupigia kura vilikuwa bado havijawasili katika vituo vyote vya kupigia kura nchini humo.

 

Video: Chadema tutaingia mtaani mchana kweupe, Kansa yamtesa Baba wa Diamond
Milioni 200 kumung'oa mbunge CUF

Comments

comments