Wakazi wa Kijiji cha Malangali Wilayani Wanging’ombe Mkoani Njombe wameiomba serikali kuharakisha kuwasogezea huduma ya maji kwani wamekuwa wakikumbwa na magonjwa ya Typhod na matumbo kutokana na kutumia maji ya mito ambayo sio safi na salama.

Wakizungumza na Dar24 Media wakazi hao wamesema wamekuwa wakitegemea maji ya mito na madimbwi wakati wa masika huku wakati wa kiangazi wamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita Nne kufuata maji mtoni.

Wananchi hao Akiwemo Yekonia Ngongomi na Shuhudia Kiswaga wamesema tatizo hilo limedumu kwa muda mrefu hali iliyokuwa ikiwasababishia magonjwa ya matumbo Kwa Kutumia Maji Machafu Ambapo katika kipindi cha kiangazi wamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita Nne kufuata maji ya mito.

“Yaani kwa habari ya maji katika kijiji chetu ni shida na mimi hapa ni zaidi ya miaka 40 tunachota maji visimani humu maji yametuama na wanyama wanayatumia hayo hayo wakati mwingine yanakuwa na wadudu, lakini sasa hivi tumeambiwa maji yanakuja na yameanza kuchimbwa tutatumia maji ya bomba kweli tutaishukuru serikali maana sisi tumekuwa wa kuugua matumbo kila wakati,”amesema mmoja wa wananchi Yekoni Ngongomi

Kwa upande wake diwani wa kata ya Malangali, Esau Sanga amesema kuwa tatizo hilo limekuwa kikwazo katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kwamba kuanza kutekelezwa kwa mradi wa maji kijijini hapo kutawaondolea adha wananchi wake ya kutembea umbali mrefu na kutumia maji machafu.

Naye Kaimu Mhandisi wa Maji Katika Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe, Frank Kaguo amesema kuwa mradi huo unaendelea kutekelezwa vizuri na huenda mkandarasi akakamilisha Kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza endapo hakutakuwa na vikwazo vingi.

Mbunge wa jimbo La Wanging’ombe Mhandisi Gerson Lwenge amesema kukamilika kwa mradi huo pamoja na ukarabati wa mradi wa mto Mbukwa inatarajiwa kukata kiu ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa wilaya ya Wanging’ombe.

 

Radi yasababisha maafa mkoani Mtwara
CCM Njombe yasema Ushindi ni lazima

Comments

comments