Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars) inaendelea na mazoezi kisiwani Zanzibar kujiandaa fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofanyika mwezi ujao nchini Congo Brazzavile.

Twiga chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage imeendelea na mazoezi kisiwani humo kwa takribani mwezi mmoja sasa kujiandaa na fainali hizo abapo imepangwa kundi A na wenyeji Congo- Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.

Mara baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Kenya (Harambee Starlets) mwishoni mwa wiki iliypita, kocha wa Twiga Kaijage ameendelea kufanyia marekebisho yalitojitokeza katika mchezo huo kwa lengo la kuhakikisha vijana wanakua vizuri kabla ya kuanza kwa fainali hizo.

Kikosi cha wachezaji 21 pamoja benchi la Ufundi na kiongozi wa msafaa wanatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi Agosti kuelekea nchini Congo-Brazzavile tayari kwa kushiriki kwa fainali hizo za Michezo ya Afrika zitakazoanza kutimua vumbi Septemba 3- 19, 2015.

Katika hatua nyingine Shirikiksho la Mpira wa Miguu chini  (TFF) limewaomba wadau, wadhamini, taasisi na mashirika mbalimbali kujitokeza kuzidhamini timu za Taifa za vijana U15 na Twiga Stars.

Twiga Stars inayokwenda kushirki fainali za michezo ya Afrika inahudumiwa na TFF pekee, hivyo ni nafasi nzuri kwa mashirika, wafanyabiashara kujitokeza kuidhamini timu hiyo ya wanawake inayokwenda kupeperusha bendera ya nchi kwenye michuano hiyo.

Aidha timu ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 pia inahudimiwa na TFF pekee katika program ya kuandaa kikosi bora kitakachoshiriki kwenye kuwania kufuzu kwa fainali za vijana Afrika mwaka 2017.

TFF peke yake haina uwezo wa kuziandaa timu hizo, hivyo inawaomba wadhamini kujitokeza kudhamini timu hizo katika progam za mapinduzi ya mpira wa miguu nchini.

Man City Wakubali Kutoa Mzigo
Neymar Kuigharimu Upya FC Barcelona