Timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars imeshindwa kufurukuta kwenye michuano ya Afrika *All African Games* inayoendelea nchini Congo Brazzaville baada ya kukubali kupoteza michezo miwili mfululizo ya kundi la kwanza.

Jana jioni Twiga Stars walikua wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Nigeria uliochezwa kwenye uwanja wa Alphonse Massemba-Débat, ambao ulidhaniwa huenda ungetoa taswira ya kiushindani katika kundi la kwanza la michuano hiyo.

Matokeo ya mchezo huo yalisomeka Nigeria 3-0 Tanzania, hali ambayo ilidhihirisha kutupwa nje kwa Twiga Stars kwenye michuano hiyo na sasa watasubiri mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya wenyeji Congo Brazzaville utakaochezwa Septemba 12.

Katika mchezo wa kwanza Twiga Stars walicheza na Ivory Coast na kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri.

Mchezo mwingine wa kundi hilo uliochezwa jana ulishuhudia wenyeji Congo Brazzaville wakikubali kufungwa Ivory Coast bao moja kwa sifuri, matokeo ambayo yameitupa nje timu mwenyeji ambayo ilikubali kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Nigeria kwa kufungwa mabao matano kwa moja.

Msimamo wa kundi la kwanza

Group A

Pos Team Pld W D L GF GA GD Pts Qualification
1  Nigeria (A) 2 2 0 0 8 1 +7 6 Knockout stage
2  Ivory Coast (A) 2 2 0 0 2 0 +2 6
3  Tanzania (E) 2 0 0 2 0 4 −4 0
4  Congo (H, E) 2 0 0 2 1 6 −5 0

Roma Apata Hofu Baada Ya Kuchia Wimbo Wake Mpya ‘Viva’
Maalim Seif, Lowassa Kuirudisha Katiba Ya Warioba