Kiungo na Nahodha wa kikosi cha Young Africans Papii Kabamba Tshishimbi amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuwaunga mkono wachezaji, badala ya kuwakejeli wanapokua ndani na nje ya Uwanja.

Tshishimbi amesema hayo alipotembelea banda la klabu hiyo lililopo katika maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara (SABASABA) yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Dar es Salaam.

Kiungo huyo kutoka DR Congo ameonyesha kuumizwa na kitendo alichofanyiwa mshambuliaji David Molinga siku za karibuni, lakini aliwajibu kwa kuikoa Young Africans kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC kwa kufunga mabao mawili na kuufanya mchezo huo uliochezwa Dar es salaam kumalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Tshishimbi amesema kuna haja ya tabia hiyo inayoonyeshwa na baadhi ya mashabiki na wanachama Young Africans ikomeshwe, na badala yake waonyeshe uungwana kwa kuwaunga mkono wachezaji.

Amewataka mashabiki na wanachama kujenga utaratibu wa kusikiliza maelezo ya timu kutoka kwa Kocha Mkuu wa klabu au viongozi wengine badala ya habari za mitandaoni, huku akiwataka kufahamu kuwa mchezaji Morrison bado ni mali ya Young Africans tofauti na inavyoelezwa.

Kuhusiana na hali yake ya kiafya kwa sasa kiungo huyo aliejiunga na Young Africans akitokea Mbabane Swallows ya Botswana mwaka 2017 amebainisha kuwa yupo salama na anaweza kucheza kwenye mchezo wa Nusu Fainali Kombe La Shirikisho (ASFC) Julai 12 dhidi ya Simba kama kocha akimpa nafasi.

Maji ya kisima yaua mifugo msibani, waombolezaji 380 wanusurika
Mwanza: Jambazi aliyevamia benki auawa na polisi