Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa atachukua hatua kali endapo itabainika kwamba Saudi Arabia imehusika na kutoweka kwa mwandishi habari wa Saudia, Jamal Khashoggi.

Khashoggi ambaye ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudi Arabia hajaonekana tangu alipoingia kwenye ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki, Oktoba 2, huku maafisa wa Uturuki wakiishutumu Saudi Arabia kwa kumuua mwandishi huyo ndani ya ubalozi.

Aidha, Trump amesema kuwa wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu kutoweka kwa Khashoggi ili kujua ukweli wa nani aliyehusika na kutoweka kwa mwandishi huyo ili waweze kutoa adhabu kali.

“Hadi sasa, wamekana na wamekataa kabisa kama wao wanahusika na kupotea kwa mwandishi, lakini kama itabainika kwamba ni wao basi Marekani itawachukulia hatua kali,” amesema Trump wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS.

Hayo yanajiri wakati ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu ambapo ameitaka Saudi Arabia kutoa ushirikiano katika uchunguzi wa kutoweka kwa Khashoggi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa wanahitaji kufahamu kilichotokea katika tukio la kupotea kwa mwandishi huyo.

Video: DataVision yashiriki mashindano ya Rotary Dar Marathon kuchangia huduma hospitali ya CCBRT
JPM anena kuhusu kuhamia Dodoma